Sunday 22nd, December 2024
@Viwanja vya Mnazi Mmoja
Kongamano la Uelimishaji na Uhamasishaji Jamii juu ya uwepo wa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu sambamba na matumizi ya nishati safi
MALENGO YA KONGAMANO
1. Elimu ya upatikanaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu itatolewa ikiwa pamoja na kujenga uelewa namna ya kusajili vikundi katika mfumo wa WEZESHA. Maafisa Maendeleo ya jamii watakuwepo kutoa huduma hii ;
2. Kutoa mafunzo juu ya umuhimu wa kutumia nishati safi sambamba na ugawaji wa majiko na mitungi ya gesi, aplon na kofia kwa mama na baba lishe 500+;
3. Elimu juu ya umuhimu wa kushiriki uchaguzi ili kuchagua viongozi wenye tija hasa katika suala zima la uwezeshaji wananchi kiuchumi;
4. Kufanya maonesho ya huduma mbalimbali za wadau wa nishati safi; na
5. Kufanya maonesho ya matumizi ya nishati safi. Jumla ya wajasiliamali 4000 wanatarajiwa kushiriki kutoka Kata zote 36 za Halmashauri na wadau wapatao 15.
KAULI MBIU: “WEKEZA KATIKA MATUMIZI YA NISHATI SAFI KWA MAENDELEO ENDELEVU NA UFANISI KATIKA KUKUZA UCHUMI”
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.