Meya wa Jiji la Itsandra nchini Comoro Mhe. Mina Lihadji ameendelea na ziara yake ya kikazi jijini Dar e salaam leo ikiwa siku ya tatu toka alipowasili.
Katika ziara yake ya leo, Meya huyo alipata wasaa wa kufanya majadiliano na baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam wakiongozwa na Meya wa Jiji Mhe. Nurd8n Bilal, na kubadilishana uzoefu ambapo baadae alipata fursa kutembelea hospitali ya Mnazi Mmoja kuona jinsi Hospitali hiyo inavyotoa huduma.
Ikumbukwe kuwa hospitali ya Mnazi Mmoja ni moja ya hospitali zinazohudumia kwa wingi wakazi wa Visiwa vya Comoro mara waingiapo nchini kwa ajili ya shughuli mbakimbali zikiwemo biashara.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.