• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaints |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Dar es Salaam City Council

  • Home
  • About Us
    • City Profile
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Council Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Department
      • Finance, Administration and Personnel
      • Works and Fire Rescue
      • Waste Management
      • Urban Planning, Environment and Transportation
      • Health Services
    • Units
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Legal and Safety
      • Public Relations and Protocol
      • Internal Audit
      • Procurement and Supply
  • Investment Opportunity
    • Tourism Activities
      • Our Dar es Salaam
      • Animal zoos
      • Cultural Arts and Traditions
      • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
      • Public spaces, Garden and Sports
      • Shopping, Entertainment and Social life
      • Historical and Heritage building and sites
      • Beaches, Waterfronts and Islands
    • Recycling of Solid Waste
  • Our Services
    • Motorcycle Permit
    • Taxi Parking Permit
    • Car Parking
    • Bus Terminals
    • Solid Waste Management
    • Land History Information
    • Burial for unclaimed dead bodies
  • Councillors
    • All Councillors
    • Standing Committee
      • Finance and Administration Committee
      • Urban Planning, Environment and Infrastructure Commitee
      • Planning and Coordination Committee
      • Social Welfare Committee
      • Ethics Committee
    • Council Meetings
    • Lord Mayor's Timetable
    • Former City Mayors
  • Projects
    • Completed projects
    • Planned Projects
    • Ongoing Projects
    • City Investments
  • Publications
    • Acts
    • ByLaws
    • Policies
    • Guidelines
    • Reports
    • Application Form
    • Integrity Pledges Form
  • Media Centre
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Speeches
    • News
    • Events

Jiji la DSM lafanya mafunzo ya Uhamasishaji wa Afua za Lishe kwa Viongozi wa Dini

Posted on: September 5th, 2024

Katika kuendelea kutekeleza Mkataba wa Lishe katika jamii, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Idara ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii leo Septemba 5, 2024 wamefanya mafunzo ya siku moja ya uhamasishaji wa Afua za lishe kwa Viongozi wa dini ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha Jamii inafahamu umuhimu wa  lishe ili kufikia adhma ya kuboresha Afya na ustawi wa Watanzania.

Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Jiji la Dar es Salaam, Afisa Afya wa Jiji hilo Reginald Mlay amewahimiza viongozi wa dini kuendelea kutumia fursa ya majukwaa ya dini kuielimisha na kuihamasisha jamii juu ya masuala ya lishe kwa watoto wa chini ya miaka mitano pamoja na kuhakikisha wananchi  wana mtindo bora wa maisha ili kufikia adhma ya kuboresha Afya na ustawi wa Watanzania.

“Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inatambua nafasi na ushawishi mkubwa wa viongozi wa dini katika jamii na ndio maana tukaona ni vyema kufanya mafunzo haya kwa viongozi wa dini kwani ni wadau muhimu wakuhamasisha na kutoa elimu ya masuala ya lishe kwa jamii hivyo Sisi kama Jiji la Dar es Salaam tutaendelea kushirikiana  viongozi wa dini kufanikisha adhima hiyo kwa kuendelea kutoa elimu na hamasa ya masuala ya Lishe kupitia majukwaa ya dini katika jamii”.Ameeleza Dkt. Mlay.

Sambmba na hilo, amewataka Wananchi kuhakikisha wanakula mlo kamili wenye virutubisho vyote muhimu vya makundi ya chakula kwa ajili ya ukuaji wa binadamu ikiwemo protini, wanga, vitamini, madini, mboga mboga, matunda na maji ili  kuimarisha afya zao na kujikinga na magonjwa yasiyoambukizwa kama kisukari na presha.

Kwa upande wake Afisa Lishe Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Flora Mgimba ameeleza kuwa lengo la mafunzo haya ni kuhamasisha na kuwajengea uwezo viongozi wa dini juu ya masuala ya lishe yanayoikabili jamii kwani viongozi wa dini wanaifikia jamii kwa ukaribu zaidi.

“Sisi kama Halmashauri tumeona viongozi wa dini ni wadau pekee wanaoweza kutumia majukwaa yao katika kuelimisha jamii juu ya masuala ya lishe kwani suala ya lishe ni mtambuka katika nchi yetu hivyo kwa kuandaa mafunzo haya tunaamini viongozi hawa wataendelea kuhamasisha na  kutoa elimu ya Lishe kwa jamii ambayo italeta matokeo chanya katika kuboresha Afya za wananchi pamoja na kupambana na changamoto ya utapiamlo ikiwemo lishe pungufu, upungufu wa vitamini,madini na lishe ya kuzidi hii ikiwa ni kuendelea kuunga mkono juhudi za  Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha inapambana na lishe duni kwa jamii ili kutengeneza kizazi chenye Afya bora kwa maendeleo endelevu ya Taifa letu”. Amehimiza Bi. Flora

Akitoa Shukrani kwa niaba ya washiriki wengine Mchungaji kutoka Kanisa la Menonite Tanzania Rev. Suleiman Orwa amesema ili kuongoza waumini katika ibada ni lazima kuongoza waumini wenye Afya bora na kuahidi kuutumia muongozo huo na mafunzo hayo katika kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusu lishe bora ili kufikia lengo la Pamoja la kuwa na jamii yenye Afya bora. "Kwenye maandiko ya Mungu biblia inasema miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu hivyo miili yetu ni sehemu ya kufanyia ibada hivyo inahitajika kuwa ni miili yenye afya nzuri, akili yenye ubunifu mzuri kwa ajili ya huduma za kiroho, hivyo baada ya kupitishwa kwenye mafunzo haya tunaahidi kwenda kuwafundisha waumini wetu”

Aidha, katika mafunzo hayo viongozi hao wameelezwa kuhusu ugonjwa wa MPOX ambao hunasababishwa na virusi aina ya Monkeypox unaopatikana kwa jamii ya wanyama ambao ni nyani, sokwe na Ngedere ambapo maambukizi haya huambukizwa endapo mtu atang’atwa na moja ya myama huyo au kugusana na mtu mwenye ugonjwa huo hivyo wananchi   kuendeleea kupewa tahadhari ya namna ya kujikinga na ugonjwa huo kwa kunawa mikono kwa maji tiririka, kuepuka kugusana kwa kupeana mikono au kukumbatiana, kuvaa barakoa pamoja na kuwahi kituo cha huduma za afya pindi wanapoona dalili za MPOX huku viongozi wa dini wakihimizwa  kuendelea kutoa elimu kwa jamii ya namna ya kujikinga na ugonjwa huo wa MPOX kwa kuzingatia kanuni za afya ikiwemo kula mlo kamili na kufanya mazoezi ili kuongeza kinga za mwili kwa kupambana na magonjwa ya mlipuko kama hayo.


Announcements

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • View All

Latest News

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • View All

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
More Videos

Quick Links

  • Former City Council Mayors
  • Motorcycle's Permit
  • Solid Waste Management
  • Smart Area
  • Dar es Salaam Centre for Architectural Heritage
  • Beaches, Waterfronts and Islands
  • Cultural Arts and Traditions
  • Historical and Heritage building and sites
  • Public spaces, Garden and Sports

Related Links

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • State House
  • Ilala Municipal Council
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Postal Address: S.L.P 20950

    Telephone: 0738 378 386

    Mobile: 0738 378 386

    Email: info@dcc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclaimer
    • Sitemap

Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.