Kamati ya Uboreshaji wa Zao la Ngozi Ngozi ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, yajipanga kuboresha zao la ngozi kuwa la Kibiashara zaidi, hayo yamebainishwa leo Novemba Mosi, 2024 na Wajumbe wa Kamati ya Ngozi wakati wa Ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi iliyotekelezwa kwa kipindi cha robo ya kwanza ambapo walitembelea na kukagua Machinjio ya Pugu maarufu kama 'Kwa Muarabu'.
Wakiwa kwenye ziara hiyo, Wajumbe waliweza kutembelea eneo la uchakataji wa ngozi lililopo katika Machinjio hayo wajumbe kuangalia uchakataji wa ngozi pamoja na kujifunza namna zao la ngozi linavyoandaliwa hadi kufikishwa sokoni.
Akiongea kwa niaba ya Mwenyekiti wakati wa ziara hiyo, Mhe. Nyansika Getama ameeleza kuwa “Ngozi ni zao la ziada linalotokana na mifugo ambalo hutumika kama malighafi muhimu katika viwanda vya ngozi na huingiza fedha nyingi za kigeni kwani kutokana na maelezo ya mchakataji inakadiriwa kuwa ngozi zote huuzwa nje hususani Nchini Nigeria na hutumika kama chakula hivyo kwa mazingira haya inabidi Kuboresha uzalishaji, ukusanyaji na usindikaji wa ngozi kwa ajili ya soko la ndani na nje ili kuongeza kipato katika halmshauri yetu kutokana na zao la ngozi."
Aidha, kutokana na umuhimu wa zao la ngozi kibiashara, Kamati imependekeza Halmashauri itenge eneo nzuri la uchakataji wa ngozi pamoja na shughuli nyingine zinazozlishwa na kutokana na zao la ngozi kwani zao hilo litakua chachu ya ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.