Na: Shalua Mpanda
Wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mikoa ya jirani, wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uchunguzi na upasuaji wa mabusha ulioanza rasmi Januari 5,2026,katika halmashauri za mkoa huo.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule amesema Serikali imegharamia matibabu hayo hivyo wananchi hawana budi kujitokeza katika maeneo yao.
Ameyataja baadhi ya maeneno ambayo huduma hiyo ya uchunguzi na upasuaji inatolewa hadi Januari 30 ni vituo vya afya Kinondoni wilaya ya kinondoni na Kilakala kilichopo wilayani Temeke.
"Tumieni siku hizi 25 zilizotolewa na Wizara ya Afya kwenda kwenye vituo hivi, wataalamu wapo wa kutosha na siku ni nyingi, wafahamisheni ndugu na jamaa wakapate huduma hii". Alisisitiza Mhe. Mtambule
Kampeni hii kwa mkoa wa Dar es Salaam inalenga kuwafikia watu 500 ambapo mpaka sasa zaidi ya watu 160 wameshafanyiwa uchunguzi na 127 kati yao wamepangiwa tarehe za kufanyiwa upasuaji
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.