Na Mariam Muhando
Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mwalimu Gift Kyando amewataka walimu wakuu wa Shule za Msingi zilizopo Jiji la Dar es salaam kuhakikisha wanasimamia misingi ya kanuni na Sheria ili wanafunzi waweze kupata elimu iliyo bora.
Ametoa kauli hiyo leo Februari 21,2026 katika kikao kazi kilichowakutanisha maafisa elimu Kata, maafisa Elimu taaluma na wakuu wa shule za Msingi kwa lengo kuimarisha sekta ya Elimu nchini.
Mwalimu Kyando amesema katika Kikao hicho wamejadili mambo mbalimbali ikiwemo mikakati ya ufundishaji na ujifunzaji, matokeo ya elimu shule za Msingi 2025, maandalizi ya mitihani ya Utamilifu "Mock" 2026 na kuwaandikisha wanafunzi wa awali bila vikwazo.
"Serikali inatarajia kupata matunda yaliyo bora hivyo mkasimamie vyema usajili wa watahiniwa ikiwa ni mwanzo wa muhula wa kwanza wa mwaka 2026 na mkazingatie Kanuni na Sheria katika kutekelezwa majukumu yenu",Alisema Kyando.
Ikumbukwe kuwa muhula wa kwanza wa masomo 2026 ulianza rasmi Januari 13,2026 hivyo kikao hicho kitakwenda kuleta tija na matokeo chanya katika sekta ya elimu Jijini hapa.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.