Madereva Jijini Dar es Salaam waaswa kujiunga na mfumo mpya wa kuegesha magari (TAUSI PARKING) ili kuwarahisishia kuweza kujua eneo la kuegeshea magari pamoja na kujua madeni yote yaliopo katika mfumo huo.
Hayo yamebainishwa Februari 03, 2025 na Meneja wa maegesho wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Neema Ngavatula wakati akizungumza na City Fm jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa mfumo wa TAUSI PARKING unamtambulisha mwenye gari pale ambapo mkusanyaji wa mapato wa eneo hilo atakapolikagua kwani kwa kufanya hivyo gari hilo halitakubali kutokana na kuwa atakuwa ashajisajiri katika mfumo huo.
Aidha, amesema kuwa mfumo huo wa TAUSI PARKING umeanza rasmi Februari 01, 2025 ambao umesaidia katika kutatua changamoto zilizokuwa zikijitokeza katika mfumo wa zamani ikiwemo mfumo kukatika, ulimbikizaji wa madeni kwa vyombo vya moto na kutokumtambua aliyemkagua.
Pia, ameeleza kuwa mfumo wa zamani ulikuwa na changamoto kwani mtu akitaka kupata eneo maalum kwa ajili ya maegesho inachukua mchakato mrefu mpaka ukamilike lakini kwa mfumo wa TAUSI PARKING inamruhusu yeyote kuomba kwa kutumia simu au kompyuta yake na ikakamilika kwa haraka na wepesi kutokana na mfumo kuwa wa kielektroniki.
Sambamba na hilo, Bi. Neema Ngavatula amesema mfumo wa TAUSI PARKING ili mtu apate eneo la maegesho ni lazima atume maombi kwa kufungua akaunti ya TAUSI PARKING itamruhusu kuingia katika mfumo huo na kukutana na moduli nne ya kwanza ni kuhusu malipo yake, kuomba maegesho ya ziada na maombi ya huduma ya vifurushi kwa kujiunga kwa siku, wiki au mwezi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.