Na: Samira Ramadhani
Mkuu wa wilaya ya Ilala, Mheshimiwa Edward Mpogolo, amekabidhi vifaa vya elimu vya kieletroniki kwa walimu na wanafunzi wenye mahitaji maalum kea lengo la kuboresha ufundishaji na ujifunzaji.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya vifaaa hivyo kwa walimu wa shule mbalimbali wilayani Ilala, Mhe. Mpogolo amesema Rais Dkt. Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa katika sekta ya Elimu kwa kuhakikisha anasimamia sual la elimu bure kwa wanafunzi, ujenzi wa miundombinu ya Elimu pamoja na mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
"Nimpongeze sana Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa vifaa vya ufundishaji kwa walimu wenye uhitaji maalumu kama kompyuta mpakato, *digital voice recorder', karatasi za kuandikia maandishi ya nukta nundu, na vingine vingi ambavyo vitaenda kurahisisha ujifunzaji na ufundishaji kwenu". Alisema.
Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam, Ndugu Elihuruma Mabelya,kwa kununua vifaa vya kujifunzia kwa mwanafunzi Ali Kimara mwenye changamoto ya maradhi adimu yanayomfanya asome akiwa kitandani kwa muda wa zaidi ya miaka nane ili kumuwezesha kuendelea na masomo kwa kiwango cha Sekondari.
Makabidhiano hayo yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya Sekindari Jangwani, yamefanyika ndani ya ahadi ya siku 100 za utekelezaji wa majukumu ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.