Na: Doina Mwambagi
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Wanawake UN Women leo tarehe 10 Aprili 2025, wameendesha mafunzo maalum kwa wataalamu wa maendeleo ya jamii pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo katika ukumbi mdogo wa Idara ya Maendeleo ya Jamii.
Lengo la mafunzo hayo ni kujadili kwa kina fursa zilizopo za kiuchumi kwa wanawake, changamoto zinazowakabili katika kuzifikia, pamoja na kuweka mikakati madhubuti ya kuzitatua.
Akiongea wakati wa mafunzo hayo, Mratibu wa Dawati la Uwezeshaji wananchi kiuchumi Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Bi. Georgis Assenga, amesema kuwa “Uwezeshaji wa wanawake kiuchumi ni nguzo muhimu katika kufanikisha usawa wa kijinsia na maendeleo endelevu ya jamii. Kuna haja ya kujenga mazingira wezeshi kwa wanawake kushiriki kikamilifu katika shughuli za utawala na kiuchumi, hasa katika ngazi ya chini na ya kati.”
Mafunzo hayo ni jitihada endelevu za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika kutekeleza ajenda ya Kitaifa na Kimataifa ya usawa wa kijinsia na maendeleo jumuishi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.