Na: Shalua Mpanda
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Albert Chalamila ameongoza zoezi maalum la usafi lililofanyika leo Januari 11,2025 katika maeneo ya katikati ya Jiji ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa viongozi wa NCHI zaidi ya 30 unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Mhe. Chalamila amesema lengo la kufanya zoezi hilo ni kuwakumbusha wananchi kufanya usafi katika maeneo yao na kuweka taswira nzuri ya Jiji la Dar es salaam katika kipindi hiki cha ugeni huo.
Akiwa katika eneo la Soko la Kimataifa la Feri, Chalamila ametoa maagizo kwa wafanyabiashara wa Soko hilo la samaki kufanya usafi ndani ya Soko hilo ambalo amedai hali yake ya usafi haitidhishi.
Amesema endapo wafanyabiashara hao hawatafuata maelekezo hayo,hatasita kulifungia Soko hilo mpaka ahakikishe hali ya usafi imeborwshwa.
Aidha, ametoa agizo kwa waendesha bodaboda na Bajaj kuwa kuanzia tarehe 20 ya mwezi huu hawataruhusiwa kuingia katikati ya Jiji ili kupunguza msongamano wa vyombo vya moto na badala yake watapewa utaratibu mzuri.
"Katika kipindi hicho cha ugeni huu mkubwa,maeneo ya katikati ya Jiji yatakuwa yakitumika na viongozi hawa wakuu wa nchi zaidi ya 30 hivyo makamanda wa mikoa ya Ilala na wengine watatangaza utaratibu mzuri hapo baadae". Alisema
Mkuu huyo wa Mkoa pia amewatahadharisha wale wote wenye tabia za wizi na udokozi kuacha tabia hiyo na hasa kipindi hiki cha ugeni wa Viongozi hao na kulinda taswira ya amani na utulivu uliopo Nchini.
Ugeni huo wa Viongozi wa Nchi na Serikali zaidi ya 30 ambao mwenyeji wake ni Rais wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan una lengo la kuzungumzia matumizi ya Nishati safi katika nchi za Afrika.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.