Wataalamu kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma leo tarehe 05 Septemba, 2024 wamefanya ziara ya siku mbili katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu katika eneo la ukusanyaji wa mapato pamoja na utekelezaji wa miradi.
Wakiwa katika Ukumbi wa Mikutano wa Mstahiki Meya Jijini humo, Wataalumu hao waliweza kujifunza namna mbalilimbali ambazo Jiji la Dar es Salaam linavyofanya kazi zake katika eneo la ukusanyaji wa mapato pamoja na kujifunza mbinu mbalimbali za kuongeza mapato pamoja na kusimamia miradi kwani kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam mapato yameongezeka kwa kasi kutokana na kuanzishwa kwa kanda za huduma ambazo zimekua chachu ya ongezeko la asimia 105% ya mapato ya ndani ya Halmashauri ukilinganisha na mwaka 2022/2023.
Akiongea wakati wa Mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Bi. Tabu Shaibu ameeleza kuwa “Napenda kushukuru ujio wenu kwani Ujumbe huu unaonesha jinsi gani Jiji la Dar es Salaam tumejiimarisha katika eneo la ukusanyaji wa Mapato hadi kuwa kivutio kwa wengine kujifunza kwetu hivyo niwaombe Wataalamu wenzetu kutoka Jiji la Dodoma mkatekeleze yote mlivyojifunza bila kusahau ushirikiano na viongozi wenu na wataalamu wengine kwa lengo la kuhakikisha tunawahudumia wananchi kwa ukaribu zaidi kwa kuzingatia ubora na utekelezaji wa miradi yetu kwa wakati ili kujenga Taifa lenye maendeleo na kukuza uchumi wa nchi yetu.”
Aidha, akiwasilisha mada mbalimbali za namna Jiji la Dar es salaam limewekeza katika ukusanyaji wa mapato pamoja na mikakati endelevu ya uwekezaji Afisa Uwekezaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bw. Mpossi Gwakisa ameeleza kuwa katika katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kwa wakati Jiji la Dar es Salaam lina mikakati ya kujenga masoko matatu ya Kisasa pamoja na Hospital kubwa tatu zitakazotoa huduma stahiki kwa wananchi na kwa gharama nafuu kabisa huku akiwasisitiza wataalamu kutoka Jiji la Dodoma kuhakikisha wanawekeza kwa lengo la kusaidia na kuwasogezea wananchi huduma muhimu karibu.
Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Jiji la Dodoma Bw. Cosmas Nsemwa amempongeza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam pamoja na watendaji wote kwa kuweza kushirikiana vyema katika kukuza mapato ya Jiji pamoja na usimamizi na utekelezaji mzuri wa miradi huku akiahidi kwenda kufanyia kazi yote waliyojifunza.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.