Sunday 22nd, December 2024
@Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul C. Makonda anawakaribisha wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam kushiriki katika kuuaga Mwenge wetu wa Uhuru kesho saa 1:30 asubuhi katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One.
Ikumbukwe kuwa Mwenge wetu wa Uhuru ulipokelewa kutoka katika Mkoa wa Lindi tarehe 27/05/2017 na kukagua miradi mbalimbali yenye thamani ya Tshs 244,392,530,334/= katika mkoa wetu kwa muda wa siku tano ambapo shughuli za kuzindua miradi mikubwa 12 zilifanyika, miradi 5 ikiwekewa mawe ya msingi, na miradi 11 ikitembelewa na kufunguliwa.
Wakazi wote wa Jiji la Dar es Salaam tujitokeze kwa wingi kuuaga Mwenge wetu wa Uhuru.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.