Na: Shalua Mpanda
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI Mhe. Reuben Kwagilwa amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinakusanya mapato ipasavyo na kufanya matumizi sahihi ya fedha.
Ametoa kauli hiyo leo Januari 3, 2026 wakati akihitimisha ziara yake ya mkoa wa Dar es salaam katika ukumbi wa Idi Nyundo uliopo katika Halmashauri ya manispaa ya Temeke.
Mhe. Kwagilwa amewataka wataalam katika Halmashauri zote kuhakikisha wanafanya kazi kww bidii na kukusanya mapato ambayo yatapelekwa katika Miradi ya maendeleo.
"Nendeni mkahakikishe mnakusanya mapato na fedha hizo zitumike ipasavyo ili ziweze kurudi katika jamii katika Miradi ya maendeleo". Alisema
Aidha, ametooa maelekezo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha fedha zinazotengwa kwa ajili ya mikopo ya asilimia 10 zinawafikia walengwa.
Naibu Waziri Kwagilwa alianza ziara ya kukagua miradi ya maendeleo mkoani Dar es salaam mwishoni mwa mwaka jana ambapo aliweza kutembelea halmashauri tano ndani ya Mkoa huu na kutoa maelekezo na ushauri katika baadhi ya Miradi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.