Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo tarehe 2 Juni, 2023 imesaini Mikataba ya Ujenzi wa Barabara ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kuzitaka kila Halmashauri Nchini Zitenge asilimia Kumi za Mapato ya Ndani kwaajili ya Uboreshaji wa Miundombinu.
Katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuzidi kuipa kipaumbele Wilaya ya Ilala amesema “Tunamshukuru sana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mpaka leo tunaona utiaji saini wa Shilingi Bilioni 6.2 kwa ajili ya Ujenzi wa barabara.
Halmashauri imetenga shilingi Bilioni 6.2 kama asilimia 10% ya mapato ya ndani katika kuteleza maagizo ya Mheshimiwa Rais na leo tumesaini mikataba ya shilingi Bilioni 5.8 kwa ajili ya ujenzi wa barabara katika majimbo matatu. Jimbo la Ukonga barabara ya Pugu - Majoe (mita 400) kitunda- Kivule (mita 500) Mwanagati - Mpalange (mita 500) jumla kilomita 1.4.
Katika jimbo la Ilala barabara za Nyati, Rufiji, mchikichini zitajengwa kwa kiwango cha lami, Mtendeni kwa kiwango cha zege ambapo gharama ni Bilioni 1.9 pia kwa upande wa Kifuru - Majoka kutakua na ujenzi wa Karavati litakalogharimu shilingi Milioni 650."
Pia Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Mpogolo amesisitiza kuwepo wa kulegalega kwa kazi kutokana na kufanya kazi kwa kujuana kwa sasa hilo suala halipo “Wito wangu kwa Upande wa TARURA tusimamie kwa umakini zaidi na kwa kushirikiana kwa kiasi kikubwa kwa upande wangu nitakuwa kila siku ninahakikisha tunasimamia miradi hii na kwa kipindi cha miezi sita kuona miradi hii inamalizika kwa wakati"
Naye, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Omary Kumbilamoto amemshukuru Rais na kuomba kwa Mkuu wa Wilaya kufikishia salamu kwa Rais wetu Mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa “Tunamshukuru sana kwa kupunguza madaraka kwa TARURA juu ya Uendeshaji wa Shughuli hizi za Ujenzi hapo awali TARURA walipewa majukumu makubwa lakini kwa sasa Halmashauri tumeweza kutafuta wakandarasi na kuweza kufuata taratibu zote kupitia Mifumo mpaka leo tunasaini Mkataba”
Pia, Mstahiki Meya amempongeza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kuweza kutenga fedha hizi pamoja na ushirikiano wake katika kuwahuisha wabunge na madiwani “Nampongeza sana Mkurugenzi na timu yake kwa kazi kubwa unayoifanya na kwa ushirikiano mkubwa unaouonesha kwa Madiwani, wabunge kuweza kufanikisha jambo hili”
Sambamba na hilo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Ndugu. SaidiSidede amesisitiza upatikani wa ajira kwa vijana sambamba na kudumisha usalama mali na vifaa katika maeneo ya ujenzi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.