Na: Shalua Mpanda
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ndugu Elihuruma Mabelya amesema Serikali imetenga zaidi ya Shilingi bilioni 10 kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya Elimu katika Jiji hili.
Amebainisha hayo wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha wakuu wa shule za Msingi na Sekondari kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee.
Mkurugenzi Mabelya amesema kiasi cha shilingi bilioni 6.2 kimetengwa kujenga na kuboresha miundombinu upande wa elimu sekondari huku kiasi cha shilingi bilioni 4.5 kikiwa kimetengwa kwa upande wa elimu msingi.
"Ni jukumu letu kuhakikisha tunakwenda kutekeleza wajibu wetu, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ameweka fedha nyingi katika Halmshauri hii ili kila kata na kila eneo lipate huduma ya elimu". Alisema
Amezitaja baadhi ya shule zilizojengwa ndani ya kipindi kifupi ikiwemo shule za sekondari Kitunda Relini, Amani, Bonyokwa, Kipunguni ambazo zimejengwa kwa mtindo wa ghorofa pamoja na shule za msingi za Olympio na Diamond.
Kikao kazi hicho ambacho kilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo na Katibu Tawala Bi. Charangwa Selemani ni maandalizi ya kuanza kwa msimu mpya wa masomo unaotarajiwa kuanza Januari 13 mwaka huu.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.