Bodi ya Afya ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam iwewataka Wakandarasi na Mafundi waliopewa tenda za Ujenzi wa vituo vya afya ndani ya Halmashauri hiyo kukamilisha Mifumo ya Umeme na Maji Ili majengo hayo yaanze kutoa huduma kwa Wananchi.
Akizungumza wakati wa Ziara Maalum ya kukagua Maendeleo ya Ujenzi wa Vituo vya Afya, Mwenyekiti wa Bodi Dkt. Irene Lema alisema kuwa lengo la ziara hiyo ni kutimiza majukumu ya Bodi ambapo bodi imeupongeza Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa usimamizi mzuri wa fedha za miradi ya afya.
"Tumefika Kituo Cha Afya Segerea ambapo Serikali imewezesha Kiasi Cha shilingi Milioni mia tano zilizotokana na tozo kwa ajili ya Ujenzi wa Majengo matano" alisema Dkt Irene
Kwa upande wake mjumbe wa bodi Ndg. Paul Matiku amesema kuwa pamoja na kujionea miradi hiyo lakini pia bodi inashauri kuharakishwa kwa ukamilishwaji wa hatua za mwisho za Majengo hayo Ili yaweze kutumika rasmi.
Naye Mganga Mfawidhi wa Kituo Cha Afya Segerea Dkt. Marry Mgusia amesema kuwa kupanda kwa gharama za Vlvifaa vya ujenzi madukani ni miongoni mwa sababu zilizopelekea kukawia kukamili kwa majengo hayo lakini mpaka sasa kila kitu kinaenda vizuri na mafundi wapo kazini kukamilisha.
Kituo Cha Afya Cha Segerea ni miongoni mwa Vituo saba vilivyojengwa ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa Mwaka wa Fedha 2021-2022.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.