Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amesema Wamepokea shilingi Bilioni 302 Kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo Wilayani huhumo.
Mhe. Mpogolo ameyabainisha hayo Oktoba 9, 2024 katika zoezi la kuweka jiwe la Msingi Shule ya Sekondari Liwiti iliopo Jimbo la Segerea Jijini Dar es Salaam ambapo amemshkuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutenga fedha hizo Kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi hiyo.
Amesema zimeshatumika shilingi Bilioni 1.7 Kwa ajili ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Liwiti ambayo Leo hii Mheshmiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. William Lukuvi ameweka jiwe la Msingi kwenye Shule hiyo ambayo imejengwa na Serikali kupitia Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM.
"Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo Wilayani hapa ni kutokana na Ushirikiano wa Viongozi walipo jijini hapa katika kuhakikisha wanatimiza adhma ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutatua changamoto zinazo wakabili Wananchi". Alisema Mhe. Mpogolo.
Kaulimbiu ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 "Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi."
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.