Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amewataka wauguzi wa Hospitali na Vituo vya Afya kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa , hayo yamesemwa leo Septemba 10, 2024 wakati akisikiliza kero za wananchi wa Kata za Zingiziwa, Msongola, Buyuni na Chanika.
Aidha, Mhe. Mpongolo amewataka wauguzi hao kutumia lugha nzuri kwa wagonjwa kwani kumuhudumia mgonjwa vizuri kunaleta faraja.
“Niwaombe wauguzi na madaktari kutumia lugha nzuri tunapowahudumia wagonjwa kwani kutumia lugha isiyo rafiki kunamfanya mgonjwa kujisikia vibaya na kuwa mnyonge, najua Kuna wagonjwa wana usumbufu kutokana na ugonjwa alionao hivyo kusababisha usumbufu kwenu hivyo niwaombe kutumia ujuzi wenu kuwatuliza kwa lugha nzuri na kuwahudumia ipasavyo.”
Sambamba na hilo, Mhe. Mpogolo ameeleza kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imejipanga kuboresha huduma za Afya kwani kiasi cha shilingi Bilioni 7 kimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa hospital itakayoboresha huduma za Afya kwa wananchi wa Jimbo la Ukonga.
“Tutapata Hospitali ya Wilaya ya kisasa kabisa , Hadi sasa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuletea fedha kwaajili ya ujenzi wa Hospitali ambapo Hadi sasa kiasi cha shilingi milion 500 zimeshatufikia kwa ajili ya kufanya taratibu zote za ujenzi wa hospitali hiyo lengo likiwa ni kuhakikisha huduma za Afya zinapatikana kwa wakati na urahisi zaidi”.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.