Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Idara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara leo Machi 29,2023 wameanza rasmi mafunzo ya kujifunza namna ya utendaji kazi ikiwa idara hiyo ni mpya.
Mafunzo hayo yanayofanyika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam yatawezeshwa kwa siku 10 na wawezeshaji mbalimbali kutoka Wizara ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMi), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), pamoja na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).
Akifungua Mafunzo hayo kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Tabu Shaibu amewataka watumishi kutoka Idara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kuhakikisha wanakua makini kusikiliza yote watakayoelekezwa katika mafunzo hayonili kuweza kufikia lengo lililokusudiwa.
Aidha Bi.Tabu Shaibu ameweza kumshukuru Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuanzaisha wizara mpya ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ambayo italeta tija katika kukuza sekta ya Viwanda na biashara nchini. “Nipende kutoa Shukrani zangu za dhati kwa Rais wetu kwa kuanzisha wizara mpya ya Uwekezaji ,Viwanda na Biashara pia niwashukuru wawezeshaji wote mlioungana na Watumishi wetu kutoka Jiji la Dar es Salaam kujitolea kuja kuwapa mafunzo haya ambayo yatakua na manufaa makubwa kwa Idara yetu kupanga mikakati mathubuti ya namna ya kuendesha biashara zetu na kuweza kukuza mapato ya Halmashauri kwa kiwango cha juu zaidi hivyo niwaombee msikilize kwa makini na nimatumaini yangu baada ya mafunzo haya mtakua mmefikia lengo lililokusudiwa”.
Vilevile Bi.Tabu Shaibu alitoa wito kwa Watumishi wa Idara ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara kuhakikisha ndani ya siku kumi za mafunzo wahakikishe wamepata walichokikusudia pia wakimaliza kazi wafanye kazi kwa kushirikiana ili kuweza kupata mafanikio ya pamoja katika kuongeza mapato ya Halmashauri ya Jiji na Nchi kwa ujumla wake.
Kwa Upande wake Afisa Biashara Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw.Amos Jeremiah ameeleza kuwa “Sisi kama watendaji wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara tumeungana na wenzetu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha tunawapa muongozo na uelewa wa namna ya utendaji kazi katika Idara mpya ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha majukumu ya kazi yanatekelezwa kwa kiwango cha juu zaidi.”
Naye Mwezeshaji kutoka Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Ishara Nzamilisi ameeleza kuwa kwa kushirikiana na Wadau kutoka BRELA na TANTRADE ni matumaini yao mafunzo haya yataenda sambamba na ilivyotarajiwa kwani mada mbalimbali zitatolewa kwa mujibu wa utaratibu lengo likiwa ni kuhakikisha sekta ya viwanda na Biashara inakua kwa kasi na maendeleo ya nchi kukua zaidi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.