Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Mizengo Kayanza Pinda leo tarehe 1 Agosti, 2023 ametembelea banda la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika Maonesho ya nane nane kanda ya Mashariki yanayojumuisha Mikoa minne ya Tanga, Pwani,Morogoro na Dar es Salaam yanayofanyika mkoani Morogoro katika Viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere kuanzia tarehe 1-8 Agusti, 2023.
Akiwa ndiye Mgeni rasmi wa ufunguzi wa maonesho hayo , Mhe Pinda ameridhishwa na teknolojia mbalimbali za Kilimo, Mifugo na Uvuvi nalizooneshwa katika banda la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kulipongeza Jiji la Dar es salaam kwa maandalizi mazuri yenye ubunifu mkubwa wa teknolojia hizo.
Katika banda hilo Mhe Pinda ameweza kuona Teknolojia mbalimbali ikiwemo Kilimo cha mbogamboga kwa kutumia Kitalunyumba,utengenezaji wa bustani za nyumbani ( home garden ), teknolojia ya uongezaji wa thamani kwenye mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi, kilimo cha uyoga na mapishi mbalimbali ya uyoga, Ufugaji wa samaki kwenye Mabwawa , Kilimo bila kutumia udongo, Utotoleshaji wa Vifaranga vya Samaki, ufugaji wa kuku , mbwa , ngombe wa maziwa pamoja na kutembelea wajasiriamali
Aidha Mhe Pinda pia amepongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kwa kuanzisha maabara maalum ya upimaji wa afya ya udongo ambayo hutumika kufundisha wakulima teknolojia mbali mbali za kilimo iloyopo Kinyamwezi katika kata Pugu.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Hashim Komba ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo amesema kuwa “kwa niaba ya Mhe Edward Mpogolo tunakushukuru sana Mhe Waziri mkuu mstaafu kwa kutembelea banda letu la Halmashauri ya Jiji , Wilaya yetu itaendelea kuwezesha vijana na wanawake ili kuongeza tija kwenye shughuli za kiuchumi wanazofanya”
Aidha Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Ushirika Ndugu Majaliwa Andrea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji ameeleza kuwa Halmashauri itaendelea kutekeleza sera za Kilimo, mifugo na uvuvi ikiwa ni pamoja na kutenga Asilimi kumi ya mapato ya ndani ya Halmashauri kuwawezesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kiuchumi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.