Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Ilala imeupongeza Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii pamoja Ustawi wa Jamii kwa kuweka mikakati mizuri ya kulinda haki za Watoto pamoja na kufuatilia tabia na mkuzi yaliyo bora Kwa Watoto.
Akizungumza Wakati wa Ziara iliyofanywa na Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya hiyo Katibu wa Wazazi Wilaya ya Ilala Ndg. Mtiti Mbasa amesema kuwa wamefanya ziara hiyo kwa lengo la kuweka uelewa wa pamoja kwakua Jumuiya ya Wazazi ndio imebeba dhima ya kusimamia malezi, elimu, mazingira, afya na utamaduni na kwamba kupitia ziara hiyo wamepata ufahamu wa kutosha na kuahidi kuwa mabalozi wa kufikisha Ujumbe Kwa wanachama walio ngazi za Matawi na Wananchi kwa ujumla.
"Tunampongeza sana Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jinsi anavyofanya kazi kubwa kuhakikisha maendeleo yanapatika. Lakini pia tunawapongeza Idara Maendeleo ya Jamii ya Jiji la Dar es Salaam kwa kutekeleza Ilani na kuweka Mipango mizuri yenye taswira ya kuiinua jamii" alisema Ndg. Mbasa
Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Wilaya ya Ilala ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam dugu George Mtambalike, amewaomba maafisa wa Maendeleo ya Jamii kufikisha taarifa muhimu zinazopaswa kuwafikia Wananchi zipite kwa Viongozi wa mitaa Ili kurahisisha ueneaji wa taarifa sahihi kuhusu maswala ya ukatili wa kijinsia pamoja na mambo mengine kwakua wananchi wote wanatoka kwenye Mitaa ambayo wao ni Viongozi hivyo ni rahisi kupeana elimu.
Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bi. Francisca Makoye amesema kuwa licha ya changamoto kadhaa ikiwemo ya Jamii kutokua na uelewa wa kutosha kuhusu maswala ya ukatili kwa watoto lakini kitengo Cha Ustawi wa Jamii Jiji la Dar es Salaam kimehakikisha elimu Inaendelea kutolewa kwa jamii pamoja na kuanzisha mabaraza ya watoto ili waweze kupata elimu ya kujiamini, kujilinda dhidi ya ukatili wa aina mbalimbali
Aidha Bi. Fransisca ameongeza kuwa kwa upande wa uwezeshaji wa kiuchumi kwa mwaka huu wa Halmashauri ya Jiji imetenga zaidi ya shilingi bilioni 6.2 kwa ajili ya kukopesha makundi ya Vijana, Wanawake na watu wenye Ulemavu.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.