Kamati ya Lishe Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo Julai 06, 2023 imefanya Kikao cha kawaida cha Kujadili taarifa za utekelezaji wa kazi za Afya na lishe kwa kipindi cha Robo ya Tatu kuanzia Januari hadi Machi 2023.
Akifungua kikao hicho kwa niaba ya Mkurugenzi, Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bw. Kheri Sultani amesema kuwa Halmashauri ya Jiji inatekeleza maagizo ya upatikanaji wa lishe kwa vitendo kwani Serikali yaTanzania imedhamiria kuendelea kulipa umuhimu wa kipekee suala la lishe bora nchini ili kuhakikisha Tanzania inakuwa na uchumi imara kupitia maendeleo ya viwanda, hivyo elimu ya Lishe itasaidia uwepo wa watu (nguvu kazi) wenye afya njema ili kuwawezesha kufanya kazi kwa bidii na Kuchochea maendeleo ya nchi.
Katika kikao hicho Divisheni mbalimbali ziliwasiliisha taarifa za utekelezaji wa kazi za Afya na lishe kwa kipindi cha robo ya tatu ambapo baada ya taarifa hizo Kamati iliweza kujadili na kutoa maelekezo kwa Divisheni ya Elimu Sekondari kuhamasisha zaidi suala la lishe kwa wanafunzi kwani inaonekana Shule nyingi za Sekondari wanafunzi hawapati mlo kamili.
Kwa upande wake Afisa Lishe wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Neema Mwakasege amesema “Kwa upande wa Divisheni ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii tumeendelea kutekeleza afua za Lishe kwa asilimia 100% huku tukifanikiwa kutoa elimu kwa Wananchi wa Kata 8 za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuhusu masuala ya lishe bora, pia kwa Kata zilizobaki kazi tutahakikisha tunazimaliza awamu ya pili ya utekelezaji.”
Aidha, katika kikao hicho wajumbe walikubaliana katika kuongeza jitihada zaidi kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi juu ya masuala ya lishe ili kuboresha Afya na kulinda Afya zao.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.