Kamati ya Ngozi ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam yaridhishwa na bidhaa zitokanazo na zao la ngozi, hayo yamebainishwa leo Mei 14, 2024 wakati wajumbe wa Kamati hiyo walipofanya ziara ya kukagua shughuli za kimaemdeleo zilizotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salam kwa Kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2023/2024 kilichoanza Januari hadi Machi 2024 ambapo wametembelea kikundi cha Chibas Leather Products kilichopo Kata ya Liwiti.
Wakiwa kwenye ziara hiyo, wajumbe waliweza kujifunza namna bidhaa hizo zinavyotengenezwa hadi kufika sokoni huku pia wakisikiliza changamoto zinazokabili kikundi hicho kusuhu upatikanaji wa zao hilo pamoja na upatikanaji wa masoko.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Moza Mwano ameeleza kuwa “Sisi kama kamati ya ngozi tunafarijika sana kuona kuwa zao la ngozi limeleta manufaa makubwa sana katika Jiji letu kwani wajasiriamali hawa wameweza kupata ajira kupitia zao hili kwa kutengeneza vitu mbalimbali kama viatu, mikanda na mapochi. Hivyo tunawapongeza kwa kazi nzuri mnazozifanya za kuhakikisha ngozi inatumika kutengenezea vitu na tutaendelea kuhakikisha zao hili tunaliboresha zaidi na linakua la kibiashara zaidi ndani na nje ya nchi pamoja na kutuingizia mapato zaidi kama Halmashauri."
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.