Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala yaridhishwa na matumizi ya fedha na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kupitia fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti CCM Wilaya ya Ilala Ndg. Said Sidde leo tarehe 14 Machi, 2023 akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Siasa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimlbali ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa mwaka 2021/2022.
Miradi iliyotembelewa na Kamati hiyo ni pamoja na ujenzi wa Kituo cha Afya Mchikichini kinachotekelezwa kwa fedha za mapato ya ndani takribani shilingi Bilioni 5.2 kikiwa hatua ya Frame Work (Boma) na hadi kufikia Novemba 2023 kituo hicho kitakamiliki,ujenzi wa ukaguzi wa mazingira ya dampo la Pugu Kinyamwezi ambapo Serikali ya Uholanzi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wametoa msaada wa Bilioni 2 kwa ajili ya uboreshaji wa udhibiti wa miundombinu ya taka ngumu, Ukaguzi wa Kivuko cha Mgeule kinachotekelezwa kwa kutumia fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo kivuko hicho kimetekelezwa kwa asilimia 54.32% na hadi kukamilika kivuko hicho kitatumia takribani shilingi milioni 614.8, ukaguzi wa ujenzi wa ghorofa lenye sakafu 5 zenye madarasa 20 na matundu 45 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Bonyokwa ambapo ujenzi huo upo hatua ya Jamvi na hadi kufikia Oktoba 2023 ujenzi unatarajiwa kukamilika na utagharimu takribani shilingi bilioni 1.7 zikiwa ni fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Ukaguzi wa barabara ya kiwango cha Lami Kasongo Mtaa wa Mafuriko yenye urefu wa mita 341 milioni ambayo imetekelezwa kwa fedha takribani shilingi milioni 456 zikiwa ni fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri.
Aidha Wajumbe hao pia walipata fursa ya kutembelea Mradi wa Kikundi cha Boda Boda TITANIC ambao ni wanufaika wa Asilimia 10% ya mapato ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambapo kwa awamu ya kwanza vijana hao walipewa shilingi milioni 12 ambazo zilitumika kununua Pikipiki tano (5) baada ya kurejesha mkopo huo wakapewa tena kiasi cha shilingi Milioni 50 ambazo wamefungua duka la huduma za miamala ya simu huku kikundi hicho kikiweza kurejesha shilingi milioni 13 mpaka sasa, aidha kikundi cha vijana ni muunganiko wa vijana saba (7) ambao walitokea mazingira magumu na wengine walikua waathirika wa madawa ya kulevya.
Akihitimisha ziara hiyo Mwenyekiti wa kamati ya Siasa Wilaya ya Ilala Ndg. Said Sidde amesema “Naipongeza sana Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa utekelezaji wa miradi kwani thamani ya fedha inaonekana pia miradi inatekelezwa kwa kiwango cha juu zaidi hii inaonyesha ni jinsi gani Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inavyotekelezwa kwa kasi zaidi.”
Sambamba na hilo Bw.Sidde ameeleza kuwa katika dampo la Pugu Kinyamwezi ambalo linaonekana kuwa na wafanyakazi takribani 600 ambao wanaokota taka kwa ajili ya viwanda hivyo ameelekeza kuwa kama ikiwezekana Halmashauri waanzishe sheria ndogo kwa ajili ya kupata mapato kwa yale makampuni yanayochukua taka kwenye dampo kwa ajili ya kuzalisha vitu mbalimbali.
Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Bi. Charagwa Selemani amemuhakikishia mwenyekiti wa kamati ya Siasa Wilaya ya Ilala kutekeleza yote aliyoyaagiza lengo likiwa ni Kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) pamoja na kusogeza huduma za kijamii karibu na Wananchi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.