Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, leo tarehe 25 Oktoba, 2022 imefanya ziara ya kawaida ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2022 /2023 ulioanzia Julai hadi Septemba 2022.
Wakiwa kwenye ziara hiyo, kamati iliweza kutembelea na kukagua miradi mitatu (3) ikiwemo ujenzi wa Kituo cha Afya cha Zingiziwa, ujenzi wa kituo cha afya Kinyerezi pamoja na ujenzi wa madarasa ya ghorofa yanayojengwa kwenye shule mpya ya Sekondari Liwiti.
Aidha, ujenzi wa Kituo cha afya Zingiziwa unagharimu kiasi cha shilingi Milioni 500 ambapo ukenzi huo ukiwa umefikia hatua ya ukamilishaji huku ujenzi wa Jengo la upasuaji ukitarajiwa kuanza hivi karibuni baada ya taratibu za manunuzi kukamillika ambapo hadi kufikia Disemba 30 majengo yanatakuwa yamekamilika na kuanza kutumika.
Sambamba na ujenzi huo ujenzi mwengine ni wa kituo cha afya Kinyerezi uliotengewa shilingi millioni 500 napo ukenzi ukiwa kwenye hatua ya ukamilishaji wa jengo la upasuaji na jengo la wazazi huku jengo la wagonjwa wa nje 'OPD' likiwa kwenye hatua ya renta na Maabara ikitarajiwa kuanza na hadi kufikia Disemba 30 majengo yote yatakuwa yamekilika na yanatarajiwa kuanza kutumika.
Kamati hiyo ilipata pia fursa ya kukagua ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa ya ghorofa 5 katika shule ya Sekondari Liwiti inayogharimu takribani shilingi bilioni 1.5 ambapo hadi kufikia Januari 2023 takribani madarasa nane ya awali kati ya 20 yatakua yamekamilika na wanafunzi kuanza kuyatumia.
Naye, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Robert Manangwa akifanya majumuisho ya ziara hiyo amesema, "Leo tumetembelea baadhi ya miradi inayosimamiwa na kutekelezwa na Halmashauri ya Jiji la DSM ambapo tumeweza kuridhishwa na utekelezaji huo japo kuna marekebisho madogo madogo yakukamilisha hususani katika Kituo cha afya kinyerezi kwani ujenzi unasuasua hautekelezwi kwa wakati."
Sambamba na hilo Mhe. Manangwa ameendelea kusema, "Ziara yetu imekua na mafanikio na nawashukuru wakuu wa idara wote pamoja na madiwani kwa kuwa watulivu na kuweza kuitekeleza ziara hii zaidi ya hayo naomba mapungufu yaliyoonekana kwenye miradi hiyo yashughulikiwe kwa wakati na kuweza kufikia hitimisho sahihi kwani tunachohitaji watu wafikiwe na huduma muhimu na bora kwa wakati"
Aidha Kamati imeridhia kuwa endapo mzabuni aliyepewa kazi ya utekelezaji wa miradi hatekelezi ipasavyo inabidi avunjiwe mkataba na mzabuni mwingine apewe kazi hiyo lengo likiwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma za jamii kwa wakati.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.