Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ilala ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo akiwa pamoja na Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Ilala wamefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleoitakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru 2023 ambapo wamekagua miradi yenyethamani ya Zaidi ya shilingi Bilioni 10 ambayo itatembelewa na Mwenge wa Uhuru Mei 27, 2023 ambapo kauli mbiu ni "Tunza Mazingira Okoa Vyanzo vya Maji kwa ustawi wa viumbe hai na Uchumi wa Taifa"
Akiongea katika ziara hiyo Mhe. Mpolo amewataka viongozi na Wataalamu kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanafanya ukaguziwa nyaraka za miradi yote itakayotembelewa na mwenge ili kujiridhisha na hatua ya utekelezaji wa mradi husika.
“Kila kiongozi katika nafasi yake anapaswa kuwajibika katikakutekeleza majukumu yake ya kazi ikiwemo na kujenga ushirikiano katika kusimamia miradi yote inayotekelezwa ngazi ya Halmshauri na kufikia lengolililokusudiwa pia mhakikishe miradi yote iliyochaguliwa kutembelewa na kuwekewa mawe ya msingi na Mwenge wa Uhuru inafanyiwa marekebisho na inatimiza sifa na vigezo vinavyotakiwa." Ameeleza Mhe. Mpogolo.
Miradi iliyoweza kutembelewa ni pamoja na eneo la mapokezi ya Mwenge wa Uhuru eneo la barabara ya Mandera, ujenzi wa barabara ya Vingunguti - Barakuda yenye Km 2.8, ujenzi wa Shule ya Sekondari Liwiti, ujenzi wa kituo cha Afya Kinyerezi, kutembelea kikundi cha vijana wanufaika wa asilimia 10% ya mapato ya ndani ya Halmashaurikinachojishughulisha na utengenezaji wa Vikoi, Ujenzi wa Kituo cha Afya Zingiziwa, shughuli za upandaji wa miti msitu wa Zingiziwa na utunzaji wa chanzo cha maji pamoja na ukaguzi wa eneo la mkesha wa Mwenge kayika viwanja vya VODP Zingiziwa.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.