Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, leo tarehe 2 Septemba, 2023 ameshiriki katika Kongamano la Wamachinga na Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kumshukuru na kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es salaam.
Akiongea wakati wa kongamano hilo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila ameeleza kwa kina changamoto mbalimbali wanazozipata vijana wa bodaboda ikiwemo ukosefu wa bima za afya kwa vijana hao, na namna yakuwasaidia vijana hao ili waweze kupata matibabu.
"Hawa madereva na wamachinga baada ya kuingia kwenye mkoa huu wa Dar es Salaam nimegundua kwamba wana mateso yao kadhaa, jambo la kwanza la muhimu madereva hawa wamepewa pikipiki lakini wanafanya marejesho na wanafanya kazi usiku mzima.
Nadhani jambo zuri lakuendelea kujadili ni namna gani tutawaokoa kutokana na maumivu wanayoyapata vijana Hawa wa bodaboda." Amesema Mhe. Chalamila
Aidha amewataka vijana hao wa bodaboda pamoja na wamachinga wote kuepuka maneno chonganishi yatakayovuruga Amani ya nchi kwani ndiyo kikwazo kikubwa kwa maendeleo yetu binafsi na taifa zima kwa ujumla.
Katika Kongamano hilo pia walishiriki viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Zungu ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ilala ambapo alieza changamoto zinazowakabili vijana wa Jimbo hilo.
"Shamba ndiyo hili tubanane hapahapa"
Kauli hii ilisemwa na Mbunge wa Jimbo hilo akimaanisha, Ili Mkoa uishi kwa amani lazima tuishi kwa kusaidiana, pia uwekwe utaratibu mzuri utakaowawezesha vijana kupata riziki na udhibiti lazma uwepo, sheria lazima zisimamiwe Ili haki na misingi ya vijana hawa ziweze kupatikana.
Hata hivyo ikumbukwe kwamba maisha ya mwanadamu yanaanza na kidogo ndipo kikubwa kinafuata, kinachohitajika ni nidhamu ya unachokipata.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.