Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita Charles leo tarehe 15 Julai, 2019 amewaongoza Wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Jiji, Mkurugenzi wa Jiji pamoja na timu yake ya Menejimenti katika ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika robo ya nne (Oktoba-Disemba) ya mwaka wa fedha 2018/2019.
Miradi iliyotembelewa katika ziara hiyo ni mradi wa ujenzi wa maduka 19 ya biashara, ukumbi wa ndani na wa nje zenye uwezo wa kuchukua watu 1,300 kwa pamoja, maeneo ya michezo ya watoto pamoja choo cha umma katika eneo la DRIMP.
Waheshimiwa Madiwani pia wamepata fursa ya kutembelea eneo la Old Boma ambako kutafanyika ujenzi wa jengo la ghorofa tano kwa ajili ya uwekezaji utakaohusisha maduka ya biashara, ofisi na nyumba za kupangisha "apartments".
Wajumbe hao wa Baraza la Madiwani wa Jiji wamempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Bi. Sipora Liana na timu yake ya Menejimenti kwa kazi nzuri iliyofanyika na kuwataka kuendelea kuboresha na kuongeza ubunifu katika uanzishaji wa vyanzo vipya vya mapato kwa lengo la utoaji wa huduma bora kwa wananchi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.