Wajumbe wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Sipora Liana akiwa na timu ya Menejimenti wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Jiji, Isaya Mwita leo tarehe 22 Machi, 2018 wamefanya Mkutano wa Baraza katika ukumbi wa Karimjee na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za kila siku na za miradi ya maendeleo kwa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2017/2018 (Oktoba-Desemba).
Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na wadau mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam wamepata fursa ya kushiriki Mkutano huo na kusikiliza mawasilisho ya taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam kutoka kwa Wawakilishi wao.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.