Katika kuhakikisha mkakati wa miaka 10 wa matumizi ya nishati safi ya kupikia unatekelezwa kwa ufanisi Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia kitengo cha Maliasili na uhifadhi wa Mazingira leo Agosti 27, 2024 wamefanya kikao na mama lishe na baba lishe kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia lengo likiwa ni kutunza Afya za watumiaji na mazingira kwa ujumla.
Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Kitengo cha Maliasili na uhifadhi wa Mazingira, Afisa Mazingira Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Neema Sita ameeleza kuwa lengo la kikao hicho ni kuwaelimisha mama lishe na baba lishe kuhama kutoka kenye matumizi ya mkaa na kuanza kutumia nishati safi ya kupikia hivyo amewataka wadau kuhakikisha wanatekeleza yote wanayoelekezwa kuhusu nishati safi ya kupikia huku akiwapongeza baba lishe na mama lishe kuwa mstari wa mbele katika kulinda mazingira kwa kuwa mabalozi wa kutumia nishati mbadala.
Mkakati wa matumizi ya nishati safi ya kupikia, ulizinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Mei 8, 2024 ukilenga kuepuka athari za matumizi ya kuni na mkaa.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.