Katika kuadhimisha miaka miwili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Leo Machi 22, 2022 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na Soko la Kimataifa la Samaki Feri wameandaa hafla maalumu ya kumpongeza na kumuunga Mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha miaka miwili ya utawala wake.
Akitoa shukrani zake za dhati kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na bodi nzima ya Soko la Kimataifa la Samaki Feri mgeni rasmi ambaye ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mussa Azzan Zungu amesema “Shughuli hii sio ndogo kwa Taifa letu kwani Hafla hii ya kumpongeza Rais wetu imefanyika bila upendeleo ukilinganisha na mambo aliyofanya katika kipindi hiki cha miaka miwili ya uongozi wake hata hivyo amekua akiwajali sana wavuvi kupitia Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kwani ameweza kutoa fedha takribani bilioni 200 kwa ajili ya kujenga Bandari ya Uvuvi Mtwara huku Milioni 37 ikitolewa kwaajili ya kununulia boti la kusaidia shughuli za ulinzi wa rasilimali za Uvuvi, Doria na uokozi katika maeneo ya fukweza.”
Sambamba na hilo Mhe. Zungu amewataka wadau wa uvuvi wote kushirikiana pamoja kupiga vita uvuvi haramu kwani huleta madhara makubwa kwenye afya za wananchi na pia uharibifu wa Mazingira.
Akisoma taarifa fupi ya Mafanikio ya Soko la Kimataifa la Samaki Feri Meneja wa Soko hilo Bw. Denis Mrema ameeleza kuwa “Mafanikio ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan yanaonekana katika kila sekta ya Huduma za Jamii, Uchumi, Miundombinu, Elimu ,Uvuvi na Siasa kwani kwa upande wa Soko Kimataifa la Samaki feri tumeweza kufanikiwa kupitia ubunifu wa Rais wetu wa kuanzisha filamu ya ‘Royal Tour’ soko letu katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wake tumeona mabadiliko makubwa kwa kuweza kupata watalii kutoka ndani na nje ya Tanzania wakitembelea soko letu." Alisema Bw. Mrema
Aidha Bw. Mrema ameendelea kusema “Katika kipindi cha miaka miwili ya Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wananchi wameweza kunufaika na mikopo ya Uvuvi kwa kuwawezesha wavuvi wadogo wadogo kupata mikopo ya zana za Uvuvi hivyo kupitia mikopo hiyo wavuvi hao wameweza kuinua kipato chao na kuimarisha utendaji wa shughuli zao.”
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.