• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

Miradi ya Shilingi Bilioni 46.8 yatembelewa na Mwenge Maalum wa Uhuru Wilaya ya Ilala

Tarehe iliyowekwa: August 19th, 2021

Na: Hashim Jumbe 

"Sisi tumekwisha uwasha Mwenge, tumekwisha uwasha Mwenge. Na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro. Kuwasha Mwenge na kuuweka Kilimanjaro" 

Naam, huo ni mpangilio wa sauti za kizalendo zilizobeba maudhui ya wimbo wa kuwashwa kwa Mwenge wa Uhuru, sauti kutoka kwa Vijana wa Halaiki wa Wilaya ya Ilala, ziliposikika asubuhi ya leo ya Tarehe 18 Agosti, 2021 kwenye viwanja vya ndege vya Dar es Salaam (terminal one) zikiashiria kuwa Mwenge wa Uhuru umewasili ndani ya viunga vya Wilaya ya Ilala

Aidha, wakati wa makabidhiano ya Mwenge huo wa Uhuru, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Luteni Mwambashi alisisitiza kuwepo kwa nyaraka na vielelezo vyote muhimu kwenye miradi ya Mwenge watakayoitembelea, huku Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija akieleza kwa ufupi miradi watakayotembelea na kuifanyia ukaguzi pamoja na kuweka mawe ya msingi "katika Wilaya ya Ilala, Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 zitapitia jumla ya miradi ya maendeleo 9 yenye jumla ya thamani ya Shilingi Bilioni 46.8"

Miradi iliyotembelewa kwa Wilaya ya Ilala ni pamoja na miradi Miwili (2) ya Vikundi vya uzalishaji mali vya vijana ambapo miradi hii imewezeshwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia  mkopo wa asilimia 10% ya mapato ya ndani pamoja na kituo cha Mifumo ya TEHAMA 'Buguruni'

Mradi mwingine ni uboreshaji wa miundombinu ya ujenzi wa barabara ya lami, Stendi ya Kinyerezi na daraja la Ulongoni B ambao umewekwa jiwe la msingi, Mradi wa ujenzi wa madarasa ya ghorofa Shule ya Sekondari Ilala-Kasulu, mradi wa ujenzi wa kituo cha Polisi Mzinga ambao umetekelezwa kwa nguvu ya Wananchi na wenyewe umewekewa jiwe la msingi.

Vilevile mradi wa afya wa wadau ambao ni ujenzi wa Hospitali binafsi ya AL-AMAL uliopo chini ya Asasi ya Direct Aid Society (DAS) inayojulikana kwa jina la Africa Muslims Agency na wenyewe umewekewa jiwe la msingi na mradi wa utengenezaji wa samani za chuma wa kikundi cha DAGE cha Watu wenye Ulemavu kutoka kata ya Vingunguti ambao umewezeshwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia  mkopo wa asilimia 10% ya mapato ya ndani, mradi huu umetembelewa na kukaguliwa na pia mbio za Mwenge zilikagua mradi wa mwaka 2019 kuona maendeleo yake,  mradi huo ni ujenzi wa Tanki la kuhifadhia maji lita Milioni 2 lililopo Pugu

Aidha, wakati akitoa Salamu na Ujumbe wa Mwenge wa Uhuru 2021 kwa Wananchi wa Wilaya ya Ilala, Kiongozi wa Mbio za Mwenge, Luteni Josephine Paul Mwambashi, Mwambashi alielezea mambo muhimu likiwemo la matumizi ya malipo ya kietroniki katika ukusanyaji wa mapato kwa ngazi ya Halmashauri, huku akiwaasa Wananchi kutokufanya malipo bila ya kupewa risiti ya EFD kwani kutokuchukua risiti kunaipunguzia Serikali mapato, lakini pia alisisitiza juu ya madhara ya madawa ya kulevya, huku akihimiza matumizi ya lishe bora ili kujenga jamii imara na kuendelea kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI ili kuikinga jamii yetu.

Mbio za Mwenge wa Uhuru 2021 zimebeba ujumbe unaosisitiza matumizi ya TEHAMA katika kuchochea maendeleo "TEHAMA ni Msingi wa Taifa Endelevu, Itumike kwa Usahihi na Uwajibikaji".

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.