Bajeti ya Halmashauri ya Jiji katika mwaka 2017/2018 imeandaliwa kwa kuzingatia Dira ya Maendeleo 2025, malengo endelevu ya millennia, Mpango wa maendeleo wa miaka mitano (5), Mwongozo wa bajeti wa mwaka 2017/2018 na maelekezo mengine ya Serikali na Halmashauri ya Jiji. Bajeti hii imejikita katika kumalizia miradi inayoendelea na kutekeleza miradi mipya ambayo inaleta tija kwa wananchi wa Dar es Salaam. Aidha bajeti ya Halmashauri imezingatia vipaumbele vifuatavyo:
Makisio ya bajeti ya mwaka 2017/2018 ni jumla ya Sh. 20,278,441,110.00 ambapo Sh. 3,133,512,000.00 ni Ruzuku toka Serikali Kuu na Sh. 17,144,929,110.00 ni makusanyo ya ndani. Aidha, kati ya mapato haya kiasi cha Sh. 6,674,688.000 ni mapato ya kugawana na Halmashauri za Manispaa na hivyo jumla ya Sh. 10,470,241,110.00 ni mapato ya ndani yatakayotumika kugharimia matumizi ya kawaida yaani matumizi mengineyo (OC), mishahara ya watumishi (PE) pamoja na miradi ya maendeleo. Jumla ya Sh. 3,377,789,976.00 zitatumika kulipia matumizi mengineyo (OC) na Sh. 530,360,968.00 zitatumika kulipa mishahara ya watumishi, Aidha Sh. 6,562,144,166.00 zitatumika kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo ni sawa na asilimia 62.67 % ya mapato yote ya ndani.
Na. |
Mchanganuo |
Jumla |
1 |
Jumla ya Mapato
|
17,144,929,110.00 |
2 |
Mapato ya Kugawa kati ya Manispaa na Wakala.
|
6,674,688,000.00 |
3 |
Mapato ya Ndani
|
10,470,241,110.00 |
4 |
Mishahara ya Ndani
|
530,360,968.00 |
3 |
Matumizi ya Kawaida
|
3,377,789,976.00 |
|
Miradi ya maendeleo vyanzo vya ndani
|
|
1 |
Ufuatiliaji na Tathmini (M & E)
|
293,107,208.30 |
2 |
Ukarabati wa barabara ya kuingia/kutoka dampo kwa kiwango cha lami yenye urefu wa 0.7km
|
600,000,000.00 |
3 |
Kukamilisha ujenzi wa ukuta wa kuzunguka Dampo (920m)
|
320,000,000.00 |
4 |
Ukarabati wa barabara za Dampo la Pugu Kinyamwezi
|
100,000,000.00 |
5 |
Kulipa fidia na kujenga miundombinu ya Dampo la Mkuranga na Kigamboni
|
1,000,000,000.00 |
6 |
Ununuzi wa maeneo na ujenzi wa vyoo vya umma
|
500,000,000.00 |
7 |
Mchango wa ujenzi wa kituo cha Mbezi Luis
|
1,035,000,000.00 |
8 |
Ukarabati wa majengo Halmashauri ya Jiji (DCC)
|
210,229,411.00 |
9 |
Kufunga camera za CCTV katika jengo kuu la Halmashauri ya jiji
|
50,000,000.00 |
10 |
Ujenzi wa vyoo vya umma na kukarabati mfumo wa umeme Karimjee Hall
|
162,447,546.70 |
11 |
Ukarabati wa miundombinu kituo cha mabasi Ubungo
|
200,000,000.00 |
12 |
Kununua eneo kwa ajili ya makaburi
|
300,000,000.00 |
13 |
Kodi ya viwanja vya Halmashauri (Land Rent)
|
250,000,000.00 |
14 |
Mikopo kwa jamii (vijana na wanawake)
|
977,000,000.00 |
15 |
Matengenezo ya mzani Dampo la Pugu Kinyamwezi
|
10,000,000.00 |
16 |
Matengenezo ya Mitambo ya kusukuma na kushindilia taka.
|
150,000,000.00 |
17 |
Gharama za uendeshaji dampo (Diesel na Petrol)
|
404,360,000.00 |
|
Jumla miradi ya maendeleo
|
6,562,144,166.00 |
2 |
Ruzuku ya Serikali Kuu
|
|
2.1 |
Mishahara
|
2,275,512,000.00 |
2.2 |
Matumizi ya Kawaida
|
- |
2.3 |
Miradi ya Maendeleo ya Ruzuku LDGD
|
850,000,000.00 |
2.4 |
Kuthibiti UKIMWI (NMSF)
|
8,000,000.00 |
|
Jumla ndogo ya Ruzuku
|
3,133,512,000.00 |
|
Jumla kuu
|
20,278,441,110.00 |
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.