• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

Mwenge wa Uhuru 2021 watembelea Mradi wa Ujenzi wa Madarasa Shule ya Sekondari Ilala-Kasulu.

Tarehe iliyowekwa: August 18th, 2021

Na: Miraji Omary

Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021, Luteni Josephine Paul Mwambashi, Tarehe 18 Agosti, 2021 alitembelea mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Ilala-Kasulu kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi katika Mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa ya ghorofa, ambao umegusa kigezo cha nne (4) kipengele cha (4.5) kinachoonesha jinsi Wilaya ilivyo wekeza na kusimamia miundombinu ya elimu. Mradi huo ambao ulianza Aprili 2019 na unatarajiwa kukamilika Mwaka huu wa fedha 2021/2022.

Mradi huo ambao unajengwa kwa Awamu Tatu na utagharimu jumla ya Shilingi Milioni 850,338,971.30 hadi utakapokamilika. Hadi kufikia sasa Mradi umefikia awamu ya Pili na fedha ambazo tayari zimekwishakupokelewa ni kiasi cha Shilingi milioni 544,054,458.32 ambapo Shilingi milioni 168,577,438.30 zimekwisha tumika katika awamu ya Kwanza na Shilingi milioni 357,477,020 zimetumika awamu ya Pili hadi ujenzi ulipofikia.

Mkuu wa shule Bw. Hamisi Ernest Masutu akisoma taarifa za mradi huo kwa kiongozi wa mbio maalum za Mwenge Luteni Josephine Paul Mwambashi amesema kuwa mradi umetumia eneo dogo kutokana na ufinyu wa maeneo katikati ya mji na kuwezesha kusajili Wanafunzi wengi, Kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani. Pia mradi umesaidia kuhudumia Watoto wa Kata zilizo karibu hivyo kupunguza umbali wa Wanafunzi kwenda shule za pembezoni kitu ambacho kimesaidia kuongeza ufaulu.

Aidha mkuu wa shule amesema wanaenda sambamba na kaulimbiu ya Mwenge maalum wa Uhuru ya mwaka 2021, isemayo “Tehama ni Msingi wa Taifa Endelevu, Itumie kwa Usahihi na Uwajibikaji” ambapo shule ya Sekondari Ilala Kasulu inatumia mifumo ya TEHAMA (PREMS, BEMIS, NA FFARS) kwa baadhi ya shuguli, ambazo imerahisisha utendaji kazi kama vile Usajili wa Wanafunzi, Uhamisho wa Wanafunzi, Uandaaji wa ripoti za Wanafunzi pamoja na Shughuli za Uhasibu kama ilivyo kwa shule zingine katika Wilaya.

Pia mkuu wa shule ameongezea kwa kusema katika shule ya Sekondari Ilala Kasulu, sekta ya elimu ipo mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya Rushwa kupitia kaulimbiu ya kudumu isemayo “Kupambana na Rushwa ni Jukumu Langu”, hivyo shule kwa kushirikiana na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU)  imeanzisha Kikundi elimishi juu ya kupambana na Rushwa mashuleni ili kujenga uelewa kwa vijana juu ya madhara yatokanayo na kutoa au kupokea Rushwa.

Sambamba na hilo Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge Kitaifa 2021, Luteni Josephine Paul Mwambashi amezindua Klabu ya kupinga na kupambana na Rushwa ya wanafunzi iliyoanzishwa kwa kushirikiana na TAKUKURU, Baada ya taarifa iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa klabu Doreen Bernad, ambapo amesema klabu hiyo inaundwa na wanachama wapatao 60, Wavulana 22 na Wasichana 38 wa Shule ya sekondari Ilala Kasulu.

Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge Kitaifa 2021, Luteni Josephine Paul Mwambashi, akihitimisha ziara yake katika mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Ilala Kasulu, amewaasa viongozi wanao simamia miradi mbalimbali kuweza kuonyesha nyaraka zote zinazo husiana na mradi husika pamoja na kushirikisha wanchi wa eneo husika iliwaweze kutambua jinsi mradi unavyo endeshwa.  

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.