Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia idara ya maendeleo ya jamii leo tarehe 29 Novemba 2022 imeendelea kutoa mafunzo juu ya ufahamu na uelewa katika mfumo wa usajili wa vikundi ambavyo vinakidhi kupata mkopo utokanao na asilimia kumi za mapato ya ndani kutoka Halmashauri kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, ambmafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Mikutano Anatoglou uliopo Mnazi Mmoja Dar es Salaam.
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inatekeleza hili kwa kiwango kikubwa kuhakikisha watendaji wa mtaa wanapata uelewa juu ya mfumo huu ili wawe mabalozi bora katika kufikisha elimu hii kwa wananchi ambao ni wanufaika wa moja kwa moja wa mikopo hii kuweza kujisajiri katika mfumo,ambapo Halmashauri imeweza kutoa kiasi cha fedha za kitanzania Zaidi Bilioni 17 na bilioni 5.8 kutoka katika marejesho kwa kipindi cha 2018/19 hadi zimetolewa kwa wananchi.Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii Bibi Francisca Makoye amesema.
“Serikali imeanzisha mfumo mpya waTPLM IS unawezesha kila kikundi kuwa na taarifa zake na unahusisha moja kwa moja wananchi na si busara kuwaacha watendaji wa mtaa na wenyeviti mfahamu mfumo huu karibuni katika mafunzo haya”
Akijibu swali la mwenyekiti wa wenyeviti Jimbo la Ilala ndugu Ally Mshauri ambaye pia ni mwenyekiti wa mtaa wa Mafuriko kutoka kata ya ilala Afisa TEHAMA kitengo cha Maendeleo ya jamii wakati anawasilisha mada amesema “Nyaraka muhimu kwa muombaji wa mikopo hii kwa vikundi ili kupata mikopo ni pamoja na barua kutoka serikali ya mtaa, barua pepe (email) ya kikundi,umri ambao kwa vijana kuanzia miaka 18-35 isizidi hapo,kwa walemavu hakuna mipaka ya umri,kikundi cha wanawake haruhusiwi mwanaume miaka hakuna mipakanamba za nida za wanachama wote ambapo wanachama kuanzia watano kwa vijana,kwa walemavu anaweza kuwa mtu mmoja tu kama maeneo hayo yuko pekee aidha kama mitaa mingine walemavu wapo wanaweza kuungana.
Mfomo huu watumiaji wakuu ni pamoja na kikundi husika,afisa maendeleo ya jamii katani, Mkuu wa idara ya Maendeleo ya jamii Mkurugenzi,Mweka azina na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam hivyo basi kikundi kinatakiwa kujisajili katika mfumo na kutuma maombi.
Nyaraka za usajili ni Pamoja na katiba,barua kutoka serikali ya mtaa hapa watendaji wote lazima wajue kikundi na wakitambue,azimio la kikundi na muhtasari wa kuomba usajili.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.