• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aongoza wananchi katika sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganika na Zanzibar

Tarehe iliyowekwa: April 26th, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 26 Aprili 2017, ameongoza maelfu ya Watanzania katika sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Maadhimisho ya Sherehe za Muungano zinafanyika mkoani Dodoma makao makuu ya Serikali ikiwa ni ishara tosha kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na chama cha Mapinduzi imedhamiria kwa dhati kuhakikisha makao makuuu ya Serikali yanakuwa Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kukagua gwaride la vikosi vya ulinzi na Usalama lililoandaliwa kwa heshima yake, Rais Magufuli amewahakikishia watanzania kuwa yeye na Rais wa Zanzibara Dkt. Ali Mohamed Shein wataendelea kuulinda Muungano kwa nguvu zao zote na kwamba atakayejaribu kuuvunja atavunjika yeye.

Rais Magufuli amesema Tanzania imeweza kufikisha miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa sababu ya amani iliyopo nchini iliyowezesha kupatikana mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuunganisha mataifa yetu mawili na kuuunda taifa moja lenye nguvu.

Aidha Dkt. Magufuli amewataka watanzania kuendelea kudumisha amani iliyopo nchini kwani amani ndio chachu ya maendeleo yanayopatikana nchini katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Mhe. Rais ametaja mafanikio mengine yaliyopatikana kutokana na Muungano ni kukua kwa uchumi na kukabiliana na matatizo ya umasikini na ukosefu wa ajira, kuimarisha miundombinu ya usafiri wa anga, majini, reli  na nchi kavu.

''Niwahahakikishie wana Dodoma na Watanzania kwa ujumla  kwamba Serikali sasa tumefika Dodoma na hatutarudi tena, na  kama tulivyoahidi mwaka 2020 Serikali yote itakuwa imehamia hapa'' amesema Rais Magufuli.

Sherehe za miaka 53 ya Muungano zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na wajane wa viongozi waasisi wa Muungano mke wa hayati Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria Nyerere na hayati Abeid Aman Karume, Mama Shadya Karume, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na viongozi wa chama na Serikali.


Kauli mbiu ya Sherehe za Muungano mwaka huu ni ''Miaka 53 ya muungano,Tuuulinde na kuuimarisha, Tupige vita Dawa za Kulevya na Kufanya Kazi kwa Bidii''

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.