simamizi Mkuu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Jiji la Dar es Salaam ndugu Elihuruma Mabelya amesema wamejipanga kuhakikisha hakuna dosari yoyote itakayojitokeza wakati wa kupiga kura na baada ya kukamilisha zoezi hilo.
Msimamizi huyo ameyasema hayo wakati akipiga kura katika kituo cha Serikali ya mtaa Karume leo Novemba 27,2024.
Amesema Halmashauri ya Jiji imejipanga kuhakikisha wananchi wanatumia muda mfupi wanapokuja kupiga kura ili waendelee na majukumu mengine
"Niwahahakikishie wananchi kuwa tumeandaa mazingira wezeshi ambayo yatamfanya Mwananchi anapofika eneo la kupigia kura anapiga kura na kuondoka mapema". Alisisitiza Mabelya.
Kwa upande wake mkazi wa eneo hilo Bi. Amina Njechele amesema zoezi la kupiga kura limeanza vizuri na hakuna changamoto yoyote aliyoipata mara baada ya kufika katika kituo hicho.
"Niwaombe tu wenzangu waache kujifungia ndani waje wapige kura,mimi binafsi nimetumia 'only five minutes' (Dakika 5 tu) kupiga kura na hapa narudi zangu nyumbani". Alisema
Zoezi la kupiga kura kuwachagua viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji linafanyika katika mikoa yote ya Tanzania Bara ambapo Serikali imetangaza siku ya leo kuwa siku ya mapumziko.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.