Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amesema hayo wakati wa zoezi maalum la usafi lililofanyika leo siku ya jumamosi Februari 01, 2025 kwa Kanda namba 1 na 2 za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuanzia eneo la Kamata, Mtaa wa Gerezani kupitia barabara ya Sokoine, Kivukoni front, Luthuli, barabara ya Barack obama kuelekea fukwe za Dengue. Usafi huo umefanyika kuanzia kuanzia saa 12:30 Asubuhi mpaka saa 4:00 Asubuhi.
"Tumekubaliana na wenzangu ili kulifanya Jiji letu kuendeleza kuwa safi na beach yetu hii kuendelea kuwa safi, Zoezi hili la usafi kwa wilaya ya Ilala ni la kila siku lakini kukutana kwa pamoja ni kila jumamosi."
Pia, Mheshimiwa Mpogolo ametoa wito kwa Wananchi, Taasisi na wadau mbalimbali wa mazingira kujitokeza katika mazoezi ya endelevu ili kuhakikisha jiji letu linaendelea kuwa safi kwa jitihada za pamoja na kwa vitendo.
Aidha, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam amesema ofisi yake itaendelea kuhakikisha upatikanaji wa vifaa vya kufanyia usafi katika mazoezi hayo kwa kushirikiana na Wakandarasi wa usafi wanaofanya kazi ndani ya Jiji la DSM.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.