Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita leo tarehe 13 Septemba, 2018 katika ukumbi wa Karimjee amewaongoza wadau mbalimbali katika kikao cha majadiliano kwa ajili ya utafiti na upembuzi yakinifu wa utekelezaji wa mradi wa mabasi ya usafiri wa wanafunzi jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo ambao umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Wakurugenzi wa Manispaa, Makatibu Tawala Wilaya, Mameya wa Manispaa, Maafisa Elimu, Wahandisi na wawakilishi kutoka kampuni ya Africarriers Limited ambayo inajihusisha na vyombo vya usafiri wa mabasi.
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika kuunga mkono Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 kwa kushirikiana na wadau imedhamiria kutekeleza mradi wa mabasi ya usafiri wa wanafunzi wa shule za Msingi na za Sekondari zinazomilikiwa na Serikali jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuboresha huduma ya elimu, kuboresha mahudhurio na kupunguza idadi ya wanafunzi wanaokatisha masomo yao kwa sababu ya adha ya usafiri.
Utekelezaji wa mradi huo mbali ya huduma bora ya usafiri, pia itachochea utoaji wa ajira kwa wafanyakazi zaidi ya 3,000 watakao ajiriwa kwenye mradi na ukusanyaji wa kodi na mapato ya Serikali wakati wa utekelezaji wa mradi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.