Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam amewaasa wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kujiepusha na tabia hatarishi ambazo zinachangia maambukizi ya UKIMWI (VVU)
Hayo aliyasema tarehe 06 Februari, 2018 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam wakati akifungua warsha ya siku mbili juu ya elimu ya UKIMWI (VVU) na magonjwa yasiyoambukiza kwa wafanyakazi na waelimisha rika katika ofisi yake.
Alisema wafanyakazi wanapaswa kuwa makini katika kusikiliza na kuzingatia mafunzo wanayopatiwa juu ya hali halisi ya VVU na UKIMWI ili kupata uelewa wa kuweza kujiepusha na maambukizi ya UKIMWI (VVU) na kuwa mabalozi katika kutoa elimu waliyopatiwa kwa wafanyakazi wengine na jamii kwa ujumla.
"Takwimu za kitaifa zinaonesha Mkoa wa Dar es Salaam kuwa na asilimia 4.7 ya maambukizi ya VVU kwa watu wenye umri kati ya miaka 15-47", alieleza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.