Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Idara ya Elimu Sekondari wakishirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania TIE leo Aprili 03, 2023 wameweza kufanya mafunzo kwa Waalimu wote wa Shule za Sekondari lengo likiwa ni kuwajengea uwezo endelevu na umahiri katika ufundishaji wao.
Mafunzo hayo yanayofanyika katika vituo mbalimbali yameweza kufunguliwa rasmi na Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Saalam Bi. Tabu Shaibu katika kituo cha Shule ya Sekondari Azania.
Aidha Akifungua Mafunzo hayo Bi. Tabu Shaibu ameeleza kuwa mafunzo haya ni muhimu sana kwa Waalimi wetu kwani kupitia mafunzo haya watafanya kazi kwa umahiri mkubwa zaidi ya hapo awali kwani mafunzo haya yatasaidia kuongezeka kwa ufaulu pamoja na kuwajengea ubunifu zaidi wanafunzi hata wanapokua wameshamaliza masomo yao ya elimu ya sekondari.
Kwa upande wake Mratibu wa Mafunzo kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) Mwl. Jivitius Sabatho ameeleza kuwa mafunzo haya yatafanyika kwa siku 4 na yanafanyika katika vituo mbalimbali ikiwemo Kituo cha Azania Sekondari, Pugu Stesheni, Pugu Sekondari, Juhudi Sekondari, Jamuhuri Sekondari, Zanaki Sekondari, Dar es Salaam Sekondari, Benjamini Mkapa Sekondari, Kisutu Sekondari, Ulongoni Sekondari pamoja na Kitunda Sekondari.
“Leo tupo hapa kufanya mafunzo kwa Waalimu wote wa shule za Sekondari za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambapo mafunzo haya yanaitwa mafunzo endelevu kazini yaliyobeba malengo makuu matatu kwanza ni kuwawezesha Wanafunzi mbinu bora za uandaaji wa shughuli mbalimbali zitakazowezesha uwezo wao katika kufundisha na kujifunza, kuwajengea uwezo wa kupima ambao ni endelevu katika hatua sote za ufundishaji pamoja na waalumu kuwajengea wanafunzi stadi nne ambazo ni kuwasiliana, ubunifu, kufikiri na kushirikiana (Collaboration, communication, critical thinking and Creativity) hivyo tunaamini mwanafunzi huyo akihitimu na hizo stadi nne ataweza kupambana na maisha kwakua hakusoma kwa lengo la kufaulu tu.” Ameeleza Mwl. Sabatho.
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule Sekondari Juhudi Mwl. Happiness Palangyo ameeleza kuwa “Tunamshukuru sana Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Idara ya Elimu Sekondari kwa kuwezesha mafunzo haya ambayo yataleta tija kwa waalimu kufundisha kufundisha kwa Vitendo zaidi pia mafunzo haya yamelenga kuinua ufaulu kwa mwaka 2023 hivyo kwa niaba ya waalimu wenzangu naamini tutatekeleza yote tutakayofundishwa ndani ya siku 4 na hatimaye kufikia Malengo.”
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.