Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amewataka wananchi wa Kata za Chanika, Zingiziwa, Msongola na Buyuni kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ili kuweza Kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuchagua viongozi bora na wanaowapenda.
Mhe. Mpogolo ameyasema hayo leo Septemba 11, 2024 wakati akizungumza na wananchi wa Kata hizo kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika viwanja vya Polisi- Gogo Jijini Dar es Salaam uliolenga kusikiliza na kutatua kero za Wananchi.
“Nipende kuwashukuru sana kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano huu ambao ni chachu ya maeneleo katika Kata zeta na Wilaya yetu, hivyo nichukue nafasi hii kuwahimiza mhakikishe mnajiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura katika makazi yenu mnayoishi kwani ili uweze kupiga kura nilazima uwe umejiandikisha kwenye daftari katika Mtaa wako husika ambao umekua unaishi hivyo nitoe wito kwenu kuhakikisha mnajitokeza kwa wingi kujiandikisha pindi zoezi likifunguliwa tarehe 11 Octoba, 2024 ili muweze kupiga kura kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa mnaowapenda na watakao leta mafanikio katika Kata zetu”. Amesisitiza Mhe. Mpogolo
Aidha, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024 sambamba na Kaulimbiu isemayo 'Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi.'
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.