Zoezi la usafi wa kila jumamosi katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam limeendelea leo Aprili 12, 2025 likiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo akiambatana na Mkurugenzi wa Jiji Ndg. Elihuruma Mabelya, Viongozi, Wakandarasi na Wananchi mbalimbali.
Zoezi hilo limefanyika katika maeneo mbalimbali ya Jiji letu kuanzia Makutano ya Kamata hadi Utumishi, Kuanzia Terminal 1 kuelekea katikati ya Mji pamoja na Fukwe za Dengu, kuanzia saa 12:00 Asubuhi.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Mpogolo amesisitiza juu ya umuhimu wa kutunza fukwe za bahari pamoja na Rasilimali za bahari zinazoweza kutumika kwa ajili ya maendeleo ya jamii yetu na nchi kwa ujumla.
Pia kufanya usafi katika fukwe za bahari kunasaidia kupambana na mabadiliko ya hali ya tabia ya nchi yanayochangia bahari kuharibika. Tutunze na kulinda rasilimali za baharini ili zitusaidie kujikwamua kiuchumi
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.