Na: Shalua Mpanda
Wataalam wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wametakiwa kushirikisha wananchi na asasi za kiraia katika kuandaa mpango mkakati kwa kipindi cha miaka mitano wa Halmashauri ya Jiji hili.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ndugu Elihuruma Mabelya wakati wa mafunzo ya siku tatu ya uandaaji wa mpango mkakati wa Halmashauri hii kwa miaka mitano kwa mwaka 2026/2031.
Mkurugenzi Mabelya amesema Halmashauri ya Jiji hili lazima na mipango yake ambayo itaendana na wakati na ili mipango iwe shirikishi ni lazima wananchi washirkishwe kuandaa mkakati huo.
"Maandalizi yetu ya ndani lazima yaakisi mpango makati wa Taifa na kila mmoja wetu afahamu kuwa anapaswa kushiriki kikamilifu katika eneo lake, sina shaka na utendaji wenu". Amesema ndugu Mabelya
Kwa upande wake mmoja wa waratibu wa mafunzo hayo Bwana Geofrey Njige ambaye ni mchumi kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam amesema mchakato wa uandaaji wa mpango mkakati huo kwa awamu ya kwanza unawashirikisha wakuu wa Idara na wataalam na baadae utapelekwa kwa wananchi na wadau wengine kwa kabla ya kupata mpango mkakati huo.
Mafunzo hayo ya siku tatu yameanza leo hii katika ukumbi wa mikutano wa hospitali ya Mnazi mmoja na yanatarajiwa kukamilika Januari 8,2026.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.