Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo Agosti 30, 2023 limefanya kikao maalumu cha kupitia taarifa ya hesabu za mwisho za Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2022/2023 uliohitimishwa Juni 30 mwaka huu ikiwa ni utekelezaji wa sheria ya fedha za Serikali za Mitaa ya mwaka 2019 sura ya 290.
Akiwasilisha taarifa za hesabu za mwisho za Halmashauri Mhasibu Msimamizi wa Hesabu za mwisho za Halmashauri Bw. Matao Alexanda amesema kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni 2023, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeandaa hesabu zake kwa mujibu wa kanuni kubalifu za utayarishaji wa hesabu, memorandamu ya fedha za serikali za mitaa, sheria za manunuzi wa umma na miongozo mbalimbali inayotolewa na Serikali.
Sambamba na hilo Bw. Matao ameendelea kusema sheria ya fedha za Serikali za Mitaa ya mwaka 2019 sura ya 290 imeelezea majukumu mahususi ya Halmashauri ambayo yamejikita katika sehemu nne, moja ni ukusanyaji wa mapato kupitia kodi, leseni, ada na tozo mbalimbali, kuonyesha matokea ya fedha zilizokusanywa kama zimetumika vizuri kwa kutayarisha hesabu zilizo sahihi, sehemu ya tatu nikutoa huduma bora kwa wananchi na sehemu ya nne ni kuleta amani utulivu na utawala bora.
Aidha Mwaka wa fedha 2022/2023 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeweza kupokea na kukusanya kiasi cha Bilioni 217 ambapo bilioni 80 ikiwa ni fedha kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali vya mapato ya ndani huku ruzuku ya miradi ya maendeleo Halmashauri imeweza kupokea jumla ya bilioni 137 na matumizi mengineyo ya uendeshaji ikiwa ni Bilioni 170.26 kwenye Mali za kudumu ni bilioni 39.6 na zilizosalia ikiwa ni bilioni 21.8.
Aidha, Bw. Matao amesema kutoka kwenye makusanyo ya ndani Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imetumia bilioni 117 kwaajili ya mishahara ya Watumishi wakati ruzuku yake kutoka Serikali kuu ikiwa ni bilioni 115 na nyingine zikiwa ni Malili ya ruzuku za wafadhili Kama MDH na mishahara ya Watumishi inayolipwa na Halmashauri.
Akiongea kwa niaba ya Mstahiki Meya Wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Naibu Meya wa Halmashauri hiyo Mhe. Ojambi Masaburi amewashukuru waheshimiwa madiwani kwa kupokea na kupitisha taarifa za hesabu za mwisho za Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2022/2023, ili ziwasilishwe katika Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa fedha za Serikali.
Aidha amewapongeza wataalamu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuweza kuandaa taarifa hizo za hesabu kwa umakini na ufanisi mkubwa huku akiwataka waendelee kukusanya mapato kwa wingi zaidi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.