Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo Leo Julai 3, 2023 amekabidhi pikipiki 36 kwa Watendaji wa Kata za Halmashauri ya Jiji lengo likiwa ni kuwarahisishia utendaji kazi katika kutekeleza majukumu yao.
Akiongea wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Ofisi za Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Mhe. Mpogolo amewapongeza madiwani pamoja na Mkurugenzi wa Jiji kwa kazi Nzuri wanayoifanya ya kusimamia mapato ambayo ndiyo yakoyopelekea kununuliwa kwa pikipiki hizo.
“Nipende kuwapongeza Madiwani pamoja na Mkurugenzi na watendaji wake kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kusimamia vizuri mapato kwani ndiyo yamepelekea kununuliwa kwa pikipiki hizi hivyo nitoe wito kwa Watendaji wa Kata kuhakikisha pikipiki hizi mnazitumia kwa matumizi sahihi ya kusimamia mapato katika Kata zenu, kusimamia miradi pamoja na kuwahudumia Wananchi pia ni matumaini yangu kwamba bajeti inayofuata tutakua tumekusanya Bilioni 100 kutoka kwenye bilioni 89 kwakuwa tumewarahisishia Usafiri na tuhakikishe pikipiki hizi hazitumiki kwaajili ya biashara kwani sio lengo lililokusudiwa."
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mhe. Omary Kumbilamoto amesema “Kutokana na ukubwa wa Jiji tulipokea maelekezo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha tunakaa na Watendaji wa Kata kujua changamoto zenu hivyo changamoto hizo tulizipokea na tumetekeleza agizo la Mhe. Rais kwani leo tutakabidhi pikipiki na mahitaji mengine yatafuata hivyo naamini kupitia pikipiki hizi tutarahisisha kukusanya mapato na kuwafikia wanachi kwa urahisi zaidi pia nitoe wito kwenukuhakikisha pikipiki hizi mnazitunza na mnazitumia kwa matumizi sahihi sio kwaajili ya biashara."
Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salam, Afisa Utumishi wa Halmashauri Bi. Bernadeta Mwaikambo ameeleza kuwa “Lengo la pikipiki hizi ni kuboresha vitendea kazi na kurahisisha utendaji kazi kwa Watendaji wa Kata hivyo Halmashauri kupitia mapato ya ndani takribani shilingi milioni 103.8 tumeweza kununua pikipiki 36 ambazo zitarahisisha utendaji kazi wenu."
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.