Na:Doina Mwambagi
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo Leo Januari 13 , 2024 amefanya ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa Kituo cha Afya Mzinga kilichopo Kata ya Mzinga Jijini Dar es Salaam.
Akiongea mara baada ya ukaguzi huo, Mhe. Mpogolo amesema lengo la Ziara hiyo ni kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inatekelezwa na kukamilika kwa wakati.
Amesema Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TTanzania ni kuhakikisha Halmashauri zote Tanzania zinakamilisha miradi yote ya maendeleo iliyokwama lengo likiwa ni wakaletea wananchi huduma za kijamii kwa ukaribu.
"Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alitoa maagizo kwa Halmashauri zote Tanzania kuhakikisha inakamilisha viporo vya miradi hivyo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, chini ya Mkurugenzi Elihuruma Mabelya na timu yake wanatekeleza agizo la Mheshimiwa Rais kwa kasi kubwa, na kituo hiki cha Mzinga ni moja wapo wa mradi uliokwama kwa takribani ya miaka 7 na sasa kimekwamuliwa na ujenzi unaridhisha kwani unakwenda kwa kasi na kwa ubora stahiki" amesisitiza Mhe. Mpogolo
Aidha, ametoa wito kwa mkandarasi anayesimamia kituo hicho kuhakikisha ujenzi unakamlika kwa wakati uliopangwa na kwa ubora unaotakikana.
Kwa Upande wake Diwani wa Kata hiyo Mheshimiwa Job Isaack amesema kituo hicho kitakua mkombozi kwa wananchi wa kata ya mzinga kwani kwa miaka mingi wamekuwa wakifata huduma za katika kata nyingine.
Ujenzi wa kituo hicho cha Afya hadi sasa kimekamilika kwa asilimia 85 na mkandarasi anatarajia kukabidhi kituo hicho mwishoni mwa mwezi wa tatu mwaka huu.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.