Maafisa Lishe kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, leo tarehe 10 Agosti, 2023 wametoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Kitunda kuhusiana na umuhimu wa Lishe bora kwa watoto na wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari zilizopo katika Kata hiyo.
Utoaji wa elimu hiyo ya Lishe ulikwenda sambamba na utoaji chanjo kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano na kuhudhuriwa na wananchi ambao ni wazazi wa wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari ambazo zipo katika Kata ya kitunda.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Afisa Tawala wa Wilaya ya Ilala Bi. Flora Mgonja amesema kuwa ili mtoto aweze kukua vizuri kimwili na kiakili na awe vizuri kitaaluma darasani ni lazima tumbo lake liwe limeshiba vizuri.
Amesema, "Ili mtoto aweze kuwa na utulivu darasani na awe vizuri kitaaluma lazima mzazi uzingatie lishe kwa mtoto wako na iwe ni kipaumbele chako".
Mnamo tarehe 29 Oktoba, 2021 Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ilizindua mwongozo wa Kitaifa wa utoaji wa huduma za chakula na lishe kwa wanafunzi shuleni wenye lengo la kuwaelekeza wadau wa elimu nchini kote namna bora ya kutekeleza utoaji wa chakula na lishe shuleni.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.