Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Suleiman Jaffo, Juni 21, mwaka huu, ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kusimamia vema ujenzi wa kituo kipya cha kisasa cha mabasi katika eneo la Mbezi Luis jijini Dar es Salaam.
"Nimeridhika, nimefarijika kwa hatua zilizofikiwa katika ujenzi, endeleeni kusimamia kwa karibu ujenzi wa kituo hiki cha mabasi", alisema Mheshimiwa Jaffo (Mb) alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho cha mabasi.
Mheshimiwa Waziri huyo pia alimtaka Mtaalamu Mshauri wa ujenzi wa kituo hicho, kampuni ya Y&P Architects, kuhakikisha ujenzi wa kituo hicho unakamilika mwezi Julai, 2020 kama ilivyopangwa.
Alisema Serikali ya Awamu ya Tano imetoa kiasi cha shilingi bilioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho, hivyo usimamizi wake unapaswa kuwa wa karibu zaidi.
Mheshimiwa Jaffo amempongeza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana na timu ya menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kazi wanazozifanya katika ujenzi wa kituo hicho ambacho ni mojawapo ya miradi mingi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika sehemu mbambali nchini.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.