Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dr. Ashatu Kijaji ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kuwawezesha wamachinga kushiriki katika maonesho ya sikukuu ya wakulima Nane Nane katika kanda ya Mashariki yanayojumuisha mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro na Da es Salaam katika Viwanja vya Mwl Julius Kambarage Nyerere vilivyopo Morogoro yanayofanyika kuanzia tarehe 1 -8 Agosti,2023.
Hayo yamesemwa leo tarehe 6 Agosti , 2023 wakati Mhe. Dr Kijaji alipotembelea banda la Jiji la Dar es Salaam sehemu ya wafanya biashara wadogo wadogo (Wamachinga) na kujionea bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na wamachinga hao ikiwa ni pamoja na Vikoi, batiki, mikoba, vikapu, vinyago , vyombo vya asili, pamoja na urembo.
Ndugu Majaliwa Andrea, Mkuu wa Divisheni ya Kilimo , Mifugo na Uvuvi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji amemshukuru Mhe .Dr Kijaji kutembelea banda la Halmashauri sehemu ya Vijana na Wanawake Wamachinga na kueleza kuwa Halmashauri imetekeleza kauli Mbiu kwa Vitengo kwa kuwawezesha Wanawake na Vijana walioko katika sekta ya chakula pamoja na walio katika sekta mbalimbali za uzalishaji ili waweze kuongoza tija katika uzalishaji na kukuza uchumi wao pamoja na uchumi wa nchi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.